Breaking

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Rayvanny adai WCB kuna video 13 hazijatoka


Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny amesema wasanii wa WCB kutoa ngoma kwa mfululizo hakuathiri chochote katika muziki wao na isitoshe wana kazi nyingi ambazo zimekamilika sinasubiri kutoka.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Unaibiwa’ ameiambia Daladala Beat ya Magic Fm kuwa kwa hesabu za haraka WCB wana video takribani 13 ambazo hazijatoka.
“Hapa ukiangalia Wasafi kuna video siyo chini ya 13 ambazo zipo, Diamond ana video zake tano, Lava Lava ana video zake mbili, Harmonize ana video zake tatu sijui, kuna msanii mpya pia ana video zake tatu hazijatoka, mwenyewe nina video zangu bado hajatoka,” amesema Rayvanny.
“Kwa hiyo tukisema tupeane muda unaweza kushangaa mwaka mzima unatoa ngoma moja,” ameongeza.
Pia amesema kuwa kadiri msanii anavyotoa nyimbo ndivyo anazidi kujulikana na kuongeza mshabiki wapya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad