Mtuhumiwa namba moja ambaye anayedaiwa kuhusika na kifo cha msanii muziki nchini Uganda, Mowzey Radio amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini humo.
Kijana Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na jeshi la polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.
Wamala alikamatwa katika eneo la Kyengera alipokuwa amejificha kwa siku kadhaa nyumbani kwa rafiki yake. Wamala amehamishiwa mjini Entebbe.
Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.
Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.
No comments:
Post a Comment