Breaking

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Young Killer na Dogo Janja ni kama vifaranga vyangu – Young Dee


Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amefunguka kwa kudai kuwa Young Killer na Dogo Janja anawachukulia kama vifaranga vyake hivyo anaweza kuvimiliki na kuvifanya vyovyote anavyotaka.


Rapa huyo ameiambia ThePlaylist ya Times FM kuwa yeye hawezi kushindana na wasanii hao kwa kuwa ni wadogo zake ambao amewaona wakati wanakuwa.
Kupitia taarifa hiyo, mkali huyo wa Utani Utani, amemuita Dogo Janja na Young Killer ni vifaranga vyake na wala hawamsumbui chochote kwenye muziki, na hata akialikwa kwenye shoo ambayo wote kwa pamoja wapo itahitaji dau kubwa sana ili aweze perfom shoo kama hiyo, kwani yeye ni mkali na ana thamani kubwa sana, na kasema ni ngumu sana kumfananisha yeye na wao.
Rapa huyo baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Bongo Bahati Mbaya’ ameachia video ya wimbo wake mpya Utani Utani ambayo inafanya vizuri katika baadhi ya vituo vya redio na runinga.
Bongo5 inafanya jitihada za kumtafuta Dogo Janja na Young Killer ili wazungumzie kauli hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad