Msanii wa Bongo Flava, Chege ameachia rasmi albamu yake ya ‘Run Town’ ambayo inangoma 14 huku akiwashirikisha wasanii 14 katika kolabo tofauti tofauti.
Albam hiyo inayopatikana kupitia YouTube, iTunes, spotify, MZIKI.com ,Wasafi.com imewakutanisha wasanii kama Chid Benz, Bill Nass, Rich Mavoko, Dija, Iyo, Mh.Temba, Malaika, Gift, Nandy, Ray C, Sanapei, Runtown, Uhuru na Diamond Platnumz.
‘Run Town’ imefanyiwa kolabo ngoma 13 huku ngoma moja tu akiwa amefanya mwenyewe na tayari baadhi ya ngoma hizo zinazopatikana katika albamu hiyo zina video.
No comments:
Post a Comment