Msanii wa filamu Bongo, JB ametaja matatizo mawili ambayo yanazikumba tamthilia za Bongo kwa sasa.
Muigizaji huyo ametaja matatizo hayo kuwa ni uandaaji wa stori ambao amedai mara nyingi zimekuwa zikijirudia na kukosa msisimko pamoja na bajeti (fedha) kuwa ndogo.
“Matatizo ambayo yalikuja kuikumba tasnia ya filamu ukiacha usambazaji ni hadithi, sasa ikiwa hadithi nyingi hazikuwa siyo nzuri wakati wa kutengeneza filamu, vipi tamthilia mbayo ni kitu kirefu?, ndio maana utaona kuna tamthilia nyingi sana ambazo zinafanywa lakini hazivumi vile kama ilivyokuwa zamani” JB ameiambia Morning Trumpet ya Azam Tv.
“Hazimfanyi mtazamaji atoke nyumbani kwake, atoroke kazini kwa sababu muda umefika, tamthilia nyingi hazikati hivyo. Halafu tamthilia inataka mtaji mkubwa kwa mfano hela niliyotumbukiza kwenye Kiu ya Kisasi nasikia kizunguzungu,” ameongeza.
Katika hatua nyingine JB ameeleza sababu ya wasanii wengi kufanya tamthilia zaidi kuliko filamu kwa sasa kwa kusema waigizaji wengi wanafanya hivyo kwa ajili ya kipato ila yeye kama producer anafanya hivyo ili kupanua wigo wa kazi zake.
No comments:
Post a Comment