Breaking

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Linah hajutii kupiga picha za utupu katika ujauzito wake


Msanii wa muziki Bongo, Linah Sanga amesema kelele za watu kipindi alichopiga picha za utupu katika ujuzito wake hazikuwahi kumuumiza kwa lolote.


Muimbaji huyo May mwaka huu alifanya photo shooting za ujauzito wake na kuziachia mtandaoni kitu ambacho wengi walikikosoa. Akizungumza na E-Newz ya EATV Linah amesema ni vigumu kumridhisha kila mtu hivyo anafanya kile anachopenda.
“Mimi hazikuniboa kwa sababu hata nikifanya kitu kizuri kuna watu watakiponda kuwa ni kibaya, huwezi ukamridhisha binadamu hata siku moja. Nitapiga picha na gauni refu nitaambiwa huo ushamba, ukipiga picha na vigauni vifupi utaambiwa upo uchi, kwa hiyo kila sehemu ina mashabiki wake,” amesema Linah.
“Kwa hiyo mimi nafanya kile ambacho nakipenda kwenye moyo wangu, na hiyo ndivyo ilivyo kama msanii au mtu maarufu lazima hiyo itokee, hawawezi wakakupenda wote,” ameongeza.
Katika hatua nyingine Linah amesema endapo siku za mbeleni atajaliwa tena mtoto huyo ndio atakuwa wa mwisho kwani hana mpango wa kuzaa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad