Msanii wa muziki Bongo, Chege ameeleza mambo machache muhimu kuhusu albamu yake mpya.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Run Town’ ambayo ndiyo inabeba jina la albamu, ameiambia Dj Show ya Radio One kuwa albamu hiyo itakuwa inapatika online pekee kwa kipindi cha mwezi mmoja na baada ya hapo itapatikana katika mfumo wa CD.
Hata hivyo katika CD kutokuwa na ongezeko la ngoma kutoka 14 ambazo zinapatika katika albamu ya online hadi 17.
“Itakuwa na bonus track tatu kati ya hizo kutakuwa na single ambayo nitaitoa, kwa hiyo kwenye CD itakuwa ni tofauti na albamu ambayo ipo online” amesisitiza.
Chege anaungana na wasanii wengine wa Bongo Flava kama Lady Jaydee na Navy Kenzo ambao wametoa albamu kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment