Mkali wa kudance na kuimba Bongo, Msami Baby anaye-hit na ngoma yake ya ‘Mdundo’ kwa sasa ameeleza kuwa moja ya sababu za kucheza staili tofauti tofauti katika nyimbo zake ni kwa sababu ya aina ya masabiki aliona.
Akiongea katika DalaDala Beat ya Magic FM, msanii huyo ameeleza kuwa ana mashabiki wengi wa kike na watoto hivyo anajitahidi ku-balance aina ya uchezaji wake katika video.
” Katika video zangu na hakikisha na gusa kila mtu ndio maana nafanya hivyo, Mimi nina mashabiki wengi wa kike ambao ni watoto, wanafunzi wa chuo na wakina mama ambao wapo wengine wananifuata kuniambia niwa fundishe kudance,” amesema msanii huyo.
Pia akaongeza katika suala la kufundisha watu kucheza “Kwa sasa nina watu kama wanne kwa ajili ya training kuwafundisha kudance ili waweze kuwa fundishe kucheza.”
No comments:
Post a Comment