Breaking

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Madee, Dogo Janja kudondosha albamu


Wasanii wa Bongo Flava kutoka Tip Top Connection, Madee na Dogo Janja wana mpango wa kutoa albamu ya pamoja.
Dogo Janja ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa album hiyo itakwenda kwa jina la Mado ikiwa ni muunganiko wa majina yao na wanatarajia kuitoa November mwaka huu.
“Album itakuja inaitwa Mado ni yangu na na Madee, unajua album ni stori, ni kama kitabu unatakiwa ukisikiliza uelewe, siyo tu nyimbo ndio maana ukifuatilia Machozi, Jasho na Damu imeelezea tu,” amesema Dogo Janja.
Madee na Dogo Janja wanaungana na Roma na Stamina (Rostam) ambao nao walitangaza kutoa albamu ya pamoja mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad