Breaking

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

Andre Iniesta aikana Barcelona


Hali ni mbaya ndani ya klabu ya Barcelona ambapo wanachama wameshaanza kutafuta saini ili kupiga kura ya kukosa imani na raisi wa klabu hiyo Josep Maria Bortomeu kutokana na mambo yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.
Pamoja na ushindi mnono wa bao 5 kwa 0 dhidi ya Espanyol lakini bado hali ni tete kwa Bortomeu na kati ya mambo yanayomuweka njia panda ni suala la mikataba mipya ya Lioneil Messi na Iniesta ambayo inakarabia kuisha.
Wiki iliyopita mashabiki wa Barcelona kidogo walianza kutulia baada ya raisi wa klabu hiyo kuwaambia wameshakubaliana baadhi ya vitu kuhusu mkataba wa Iniesta na siku si nyingi kiungo huyo mkongwe atasaini.
Lakini kwa kauli yake Andre Iniesta amesema hajawahi kukubaliana kitu chochote na Barcelona kuhusu mkataba wake mpya, “inafahamika kukiwa na misingi ya makubaliano kila kitu kinakaribia kukamilika, lakini hadi sasa hakuna makubaliano yoyote” Iniesta.
Iniesta amesisitiza kwamba pamoja na yote yanayoendelea hivi sasa ndani ya klabu hiyo lakini yeye nia yake ni kucheza katika kiwango cha hali ya juu na kuisaidia klabu yake hiyo aliyoitumikia tangu mwaka 1996.
“Sijui lini nitafanya maamuzi na sijawahi kuwaza hilo, kichwa changu,mwili wangu kuna siku utafanya maamuzi, hapa ni nyumbani kwangu na hali ndio kama ilivyo tutaona nini kitatokea” alisema Iniesta.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad