Breaking

Post Top Ad

Monday, May 21, 2018

MWANAFUNZI AFARIKI KWA KULIPUKIWA NA BETRI YA SIMU MWANZA

Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo ambapo amesema limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.

“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake," amesema Kamanda Msangi.


Aidha Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa watoto hao walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtoto mwingine aliyejeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad