Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa mishahara ya wiki mbili mshambuliaji wake, Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Makato ya fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalumu nchini humo kama sera ya klabu ya Everton ya kusaidia watu wasiojiweza.
SOMA ZAIDI – Wayne Rooney ashushiwa ‘rungu zito’ na mahakama
Wayne Rooney ambaye anapokea kiasi cha Euro 150,000 kwa wiki itamlazimu kukatwa Euro laki 3, sawa na shilingi milioni 805 za kitanzania.
Mahakama nchini Uingereza siku ya Jumatatu ilimuhukumu Wayne Rooney kutoendesha gari kwa miaka miwili na kufanya kazi za kijamii kwa masaa 100 baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari akiwa amelewa.
No comments:
Post a Comment