Msanii wa muziki Bongo, Q Boy Msafi amebainisha kuwa alianza kutumia jina hilo kabla ya kuanza kufanya kazi na WCB.
Muimbaji huyo hapo awali alikuwa mbunifu wa mavazi wa msanii Diamond Platnumz ambaye ndiye mmiliki wa WCB kabla ya kuondolewa katika label hiyo.
“Hilo jina nilikuwa nalo kwa sababu mimi kama mimi since day one kabla ya muziki na kila kitu, yaani mtu yeyote alikuwa akiniona dah mshikaji msafi!! hiyo ni introduction yangu. Ni mtu ambaye napenda kupenda vizuri na ndio watu wakaniita lile jina kutokana walikuwa wananiona,” Q Boy ameiambia Entertainment live ya Azam Tv.
Q Boy Msafi kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Unaanzaje’ akiwa ni ngoma yake ya tatu kutoa tangu kuanza muziki.
No comments:
Post a Comment