Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka amefunguka na kusema kuwa CCM hakihusiki kivyovyote vile na kutekwa kwa mgombea wa Udiwani wa CHADEMA Kata ya Buhaganza , Nelson Athanas ambaye alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui.
Tibaijuka amedai kuwa kuwekuwepo na tetesi kuwa chama chake kimehusika na kitendo hicho cha kinyama na kudai kuwa hilo ni lengo la kutaka kuvuruga uchaguzi huo hivyo amesisitiza kuwa chama chake hakihusiki na unyama huo.
"Kamati ya siasa ya wilaya ya Muleba imeamua kuwajulisha wananchi rasmi na wapiga kura wa Kata ya Buhaganza na Umma wa Watanzania kiumjula kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiusiki kwa lolote lile na tuhuma hizo zinazoongozwa kwake na viongozi wake kwa nia mbaya ya kuwachafua na kukichafua chama na kuvuruga uchaguzi baada ya kuzidiwa, CCM kimejitayarisha vyema kwa ushindani na kinaamini mgombea wake Bi. Jenitha Tibihenda anatosha hivyo hakuna haja ya kumteka mshindani wake yoyote yule tupo imara" alisema Tibaijuka
Aidha Tibaijuka alivitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa tukio hilo kwa haraka ili watu waliotenda tukio hilo ovu waweze kupatikana kwa haraka na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mgombea wa udiwani Kata ya Buhangaza, Muleba (CHADEMA), Athanasio Makoti aliyekuwa amepotea tangu Februari 2, 2018 alipatikana Februari 5, 2018 akiwa hajitambui, CHADEMA imesema alitupwa barabarani maeneo ya Hospitali ya Kagondo na sasa aendelewa kupatiwa matibabu.
No comments:
Post a Comment