Breaking

Post Top Ad

Monday, May 21, 2018

Lionel Messi ashinda tuzo na kuweka rekodi barani Ulaya



Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana usiku amemaliza mchezo wake wa mwisho wa La Liga kwa msimu huu kwa kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu barani Ulaya.

Lionel Messi
Messi amemaliza msimu wa mwaka 2017/18 akiwa na magoli 34 na kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika ligi zote kubwa barani Ulaya akimuacha mshindani wake Mohamed Salah wa Liverpool kwa magoli mawili (32) .
Hii ni mara ya tano kwa mshambuliaji huyo Muajentina kuchukua tuzo hiyo na kuweka rekodi ya mchezaji wa kwanza barani Ulaya kuchukua kwa wingi tuzo hiyo kwa muda wote.
Kwenye mchezo huo wa jana Barcelona waliibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Real Sociedad na goli hilo pekee la ushindi lilifungwa na Phillippe Coutinho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad