Mugizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amesema hana bifu lolote na Harmonize mara baada ya muimbaji huyo kumtaja mume wake Chid Mapenzi katika orodha ya wanaume ambao alidai wamewahi kutoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.
Muigizaji huyo amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.
Soma Pia: Harmonize ataja list ya wanaume 12 waliotembea na Jacqueline Wolper
“Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao,” amesema.
“Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu,” Shamsa ameiambia FNL ya EATV.
Soma Pia: Shamsa Ford akiri kuumizwa vikali na Harmonize (+Video)
Usiku wa kuamkia May 8, 2018 ndipo Harmonize alitoa orodha hiyo ya Wolper ambaye ni ex-girlfriend wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, hata hivyo Shamsa alimjibu kwa wakati huo na kumueleza kuwa Chid kwao anaweza kuwa mshikaji ila kwake ni mume, hivyo ni muhimu kuheshimiana.
No comments:
Post a Comment