Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Kaimu Rais wake, Salim Abdallah ‘Try Again’ umemkabidhi zawadi ya jezi yenye namba 19 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Abdallah amesema kuwa zawadi hiyo kwa Rais Magufuli ilipaswa kutolewa Jumamosi lakini kutokana na ufinyu wa ratiba namna ilivyokuwa ulishindwa kumpatia.
Simba wamemkabidhi jezi hiyo Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, kufuatia kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa juzi kati ya Simba dhidi ya Kagera Sugar.
Magufuli alihudhuria mchezo huo wa ligi na kupata fursa ya kuwakabidhi Simba kombe la ligi walilotwaa msimu huu.
Simba wamempa jezi hiyo Waziri Mwakyembe amfikishie Magufuli wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Katiba uliokuwa unafanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment